RAIS SAMIA AANZA ZIARA YA SIKU TATU ANGOLA

ccmkwanza
1 Min Read

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa  4 De Fevereiro Luanda kwa ajili ya Ziara ya Kiserikali ya siku 3 nchini Angola tarehe 07 Aprili, 2025. Rais Dkt. Samia amealikwa na Rais wa Angola Mhe. João Manuel Gonçalves Lourenço na lengo la Ziara hiyo ni kukuza na kuimarisha zaidi mahusiano ya kihistoria na kidugu baina ya Tanzania na Angola.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Angola  Mhe. Téte António mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa 4 De Fevereiro Luanda kwa ajili ya Ziara ya Kiserikali ya siku 3 nchini Angola tarehe 07 Aprili, 2025.

Share This Article
Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *