MAMBO YAMEANZA CCM, DKT. SAMIA ACHUKUA FOMU ZA KUOMBA KUWANIA URAIS

ccmkwanza
1 Min Read

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele akimkakabidhi mkoba wenye fomu za kuomba kuteuliwa kuwa Mgombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan. Mgombea huyo wa CCM alichukua fomu hizo leo Agosti 9,2025 ambapo Tume inataraji kufanya uteuzi Agosti 27 mwaka huu.  

Dkt. Samia Suluhu Hassan na Dkt. Emmanuel Nchimbi wakionesha mkoba wenye fomu hizo.

Dkt. Samia akipongezwa na ndugu yake.

Wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa  CCM.

Msafara ulipokuwa unaingia Makao Makuu ya INEC Njedengwa, Dodoma.

Baadhi ya viongozi wa CCM wakiwa eneo la tukio.

Baadhi ya viongozi wanawake wa CCM.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Salim Asas akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa UWT Taifa, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu, Mary Chatanda walipokuwa wakisubiri wagombea kuwasili kuchukua fomu hizo katika Makao Makuu ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi.

Dkt. John Nchimbi Katibu Mkuu wa CCM, ambaye pia ni Mgombea Mwenza wa Urais, akizungumza na baadhi ya viongozi wa CCM.

Share This Article
Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *