Mgombea wa Nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan ahutubia wananchi wa Njombe katika muendelezo wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu kwa Chama hicho mkoani humo tarehe 05 Septemba, 2025.
Ameahidi kufufua baadhi ya viwanda vya chai vilivyosimama uzalishaji na wakulima wa parachihi kuwajengea vituo 50 vya kuhifadhia matunda hayo hadi miezi mitatu kabla ya kusafirishwa kwa mauzo nje ya Nchi.