KAMPENI ZA DKT. SAMIA ZAHAMIA ZANZIBAR

ccmkwanza
1 Min Read

 Baada ya uzinduzi wa kampeni kwenye viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe Jijini Dar es Salaam Agosti 28, 2025, leo Septemba 17, 2025 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anaingia kwa kishindo Tanzania Visiwani  baada ya kufanikisha kwa kiwango cha hali ya juu kampeni zake Tanzania Bara katika mikoa tisa ya Morogoro, Dodoma, Songwe, Mbeya, Njombe, Iringa, Singida, Tabora na Kigoma.

Leo Jumatano anatarajia kufanya mikutano mikubwa  ya pamoja na Mgombea Mwenza, Dkt. Emmanuel Nchimbi asubuhi hii eneo la Unguja, Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi baada ya hapo watafanya eneo la Mwehe,Wilaya ya Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja na baadaye eneo la Nungwi Wilaya ya Kaskazini A, Mkoa wa Kaskazini Unguja. 

Alhamisi Septemba 18 Dkt. Samia ataendelea na kampeni eneo la Nungwi, Wilaya ya Kaskazini A, Mkoa wa Kaskazini Unguja na Ijumaa Septemba 19, 2025 atafanya mambo kwenye Uwanja wa Gombani ya Kale, Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba.

Share This Article
Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *