Na Richard Mwaikenda, Buhongwa, MWANZA
Mkoa wa Mwanza wameahidi kumpatia ushindi wa kishindo Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika majimbo yote 9 ya Uchaguzi.
Ahadi hiyo imetolewa kwa niaba ya wananchi na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa huo, Michael Masanja alipokuwa akitoa salamu za Mkoa kumkaribisha Dkt. Samia mkoani humo katika mkutano wa Kampeni uliofanyika Kata ya Buhongwa, Nyamagana Oktoba 7, 2925.
Amesema kuwa wananchi watampatia ushindi huo kutokana na kuuletea Mkoa huo maendeleo makubwa yanayoonekana na kila mtu.
Serikali inayoongozwa na Rais, DKT. Samia imepeleka mkoani humo zaidi ya sh. 5 za ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo miundombinu ya barabara, afya, elimu, maji, Kilimo, nishati na mawasiliano.
Leo, Dkt. Samia amefanya kampeni pia Wilaya ya Misungwi na Sengerema ambapo katika mikutano hiyo alijinadi yeye, wagombea ubunge na madiwani wa CCM. Kesho Oktoba 8 atafanya kampeni katika mkutano mkubwa utaofanyika jijini Mwanza.