BALOZI MIGIRO AKUTANA NA MKUU WA MISHENI YA SADC

ccmkwanza
1 Min Read

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Asha-Rose Migiro, amekutana na Mhe. Richard Msongwa, Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Malawi na Mkuu wa Misheni ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika (SADC). 

Mazungumzo yao yamehusu maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania unaotarajiwa kufanyika tarehe 29 Oktoba 2025.

Jopo la Waangalizi wa Uchaguzi kutoka Jumuiya ya Maendeleo kusini mwa Afrika (SADC) lipo nchini kufuatilia hatua za maandalizi ya uchaguzi huu wa saba tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, ikiwa ni kielelezo cha uimara wa demokrasia nchini. 🇹🇿🗳️

Share This Article
Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *