60,000 WAITWA JKT KUPATIWA MAFUNZO YA UZALENDO, UTAYARI WA KULIJENGA, KULITUMIKIA TAIFA

ccmkwanza
1 Min Read

MKUU wa Jeshi la Kujenga Taifa Meja Jenerali Rajabu Mabele amewataka wahitimu wa kidato cha sita Tanzania Bara na Visiwani waliochaguliwa kujiunga na mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria kuripoti katika makambi waliyopangwa ili waweze kujengewa uzalendo,ukakamavu ,kufundishwa nidhamu,Umoja wa Kitaifa,Stadi za kazi na utayari wa kulijenga na kulitumikia Taifa lao. Akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba yake, leo Mei 28,2026 Makao Makuu ya JKT mkoani Dodoma, Mkuu wa Tawi la Utawala JKT Brigedia Jenerali Hassan Mabena amesema majina ya waliochaguliwa yanapatikana kwenye tovuti ya JKT ambayo ni www.jkt.mil.tz.

Mkuu wa Tawi la Utawala JKT Brigedia Jenerali Hassan Mabena akizungumza na vyombo vya habari.

Share This Article