Mgombea kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama hicho, Dkt. Samia Suluhu Hassan yupo mguu sawa kesho Jumatano Septemba 3, 2025 kuanza kampeni katika Mkoa Songwe.
Akiwa mkoani humo atafanya mikutano katika mji wa Tunduma na Vwawa kwa kuwaomba wananchi ridhaa ya kuchaguliwa katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 29, 2025 na kuwanadi wagombea ubunge na madiwani wa chama hicho pamoja na kunadi Ilani ya Uchaguzi ya chama hicho ambapo pia ataelezea mafanikio yaliyopatikana ndani ya miaka minne ya uongozi wake pamoja na kutoa ahadi ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Hapa ni baadhi ya miradi iliyotekelezwa na inayoendelea kutekelezwa katika Mkoa huo kitinda mimba wa 26
na mchanga zaidi Tanzania lakini kwa upendo wake Rais ameupa upendeleo mahsusi.
1.Ujenzi wa barabara kuu ya Tanzam Kwa njia 4 kuanzia Igawa(Mbeya) Hadi Tunduma(Songwe) km 218
2.Ujenzi wa barabara ya Ruanda/Iyula (Tanzam Jnct)-Nyimbili-Itumba-Isongole(Malawi Border) km 79.6
3.Ujenzi wa barabara ya Mahenje-Vwawa km 32
4.Ujenzi wa barabara ya Mlowo-Kamsamba km 130 &Utambalila-Chitete Bypass
5.Makongolosi-Chang’ombe-Mbalizi
6.Isongole-Isoko km 52
7.Ujenzi wa Tunduma Dry Port(Mpemba)
8.Miradi wa Uchimbaji Madini Adimu(Ngualla Rare Earth Project)
9.Mradi Wa Uchimbaji wa Dhahabu Wilaya ya Songwe
10.Ujenzi wa Maegesho ya Kisasa ya Malori Chimbuya.
–
11.Ujenzi wa Vwawa-Mpemba-Nkangamo Bypass
12.Ujenzi wa Chuo Cha Mifugo Mbozi
13.Iboya Onestop Inspection Centre
14.Ujenzi wa Makao Makuu ya TRA & TanRoads
15.Ujenzi wa Mradi mkubwa wa Umeme wa Grid ya Taifa kuunganisha na Zambia Mbeya-Tunduma-Sumbawanga kv 400
16.Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Songwe
17.Tawi la Chuo Cha Ufundi DIT Myunga Campus
18.Ujenzi wa Hospitali mpya ya Wilaya ya Ileje.
19.Mradi wa Maji Itumba-Isongole
20.Ujenzi wa Chuo Cha VETA cha mkoa
Miradi aliyoikamilisha Rais Samia ni;
-Ujenzi wa Hospital ya Mji Tunduma
-Ujenzi wa barabara ya Mpemba/Tunduma-Isongole km 50
-Ujenzi wa Makao Makuu ya Wilaya ya Momba,Songwe na Mbozi DC
-Ujenzi wa Makao Makuu ya Mkoa Bwawa
Miradi ambayo Iko mbioni ‘pipeline’ ni;
-Upembuzi yakinifu wa Vwawa na Tunduma Bypass
-Upembuzi yakinifu wa mradi mkubwa wa Maji kutoka Mto Momba Hadi Tunduma,Bwawa na Mlowo (over 320bln)
-Songwe Airport
-Songwe River Hydropower Project.
Miradi hiyo mikubwa itakapokamilika itainua uchumi wa Mkoa wa Songwe na kuleta ustawi kwa wananchi wake na Taifa Kwa ujimla.
Dkt. Samia ambaye mgombea wake Mwenza ni Dkt. John Nchimbi baada kufanya uzinduzi wa kampeni katika viwanja vya Tanganyika Packers Kawe, Dar es Salaam Agosti 28, 2025, tayari ameshafanya mikutano mingine ya kampeni katika mikoa ya Morogoro katika miji ya Ngerengere, Morogoro Mjini, Mvomero, Gairo na Dodoma katika miji ya Kibaigwa, Chamwino, Chemba, Kondoa na Dodoma Mjini.
Septemba 4-5, 2025 ataendelea kupeperusha bendera katika Mkoa wa Mbeya katika Mji wa Mbarizi na Mbeya Mjini katika Uwanja wa Ndege wa zamani eneo la Mwanjelwa. Siku yake ya pili atafanya mikutano Rungwe Mashariki,wilayani Mbarari katika Mji ya Ubaruku na Igawa baada ya hapo ataelekea mkoani Njombe.


IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
MHARIRI
BLOG YA TAIFA YA CCM
0754264203