MGOMBEA Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema, Serikali iko mbioni kujenga vituo 50 vyenye mitambo ya ubaridi wa kuhifadhia Matunda ya parachichi kabla ya kusafirisha kuuza Nje ya Nchi. Viwili vinajengwa walayani Rungwe.
Dkt. Samia ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama hicho, amesema vituo hivyo vitakuwa na uwezo wa kuhifadhia parachichi kwa miezi mitatu kabla ya kusafirishwa, lengo likiwa ni kulinda bei ya zao hilo inayobadilika mara kwa mara kutokana na wakati mwingine kuwa parachichi nyingi katika masoko ya nje.
Aidha, amesema kuwa serikali anayoiongoza imetoa miche milioni moja kwa bei ya ruzuku, lakini vilevile itatoa bure dawa aina ya Coper ya kunyunyizia kwenye miche hiyo ili kuongeza uzalishaji wa zao hilo.
Tanzania ni ya tatu kwa uzalishaji wa zao hilo, ya kwanza ikiwa Afrika Kusini na Kenya. Mikoa inayozalisha kwa wingi zao hilo nchini ni; Mbeya, Njombe na Iringa.
Amesema endapo Wananchi watamua kumpa ridhaa tena ya kuongoza Nchi kwa miaka mingine mitano kwa kumchagua katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 29, 2025, atahakikisha anakamilisha miradi yote ya Maendeleo iliyomo katika Ilani ya Chama hicho.
Wakati huo huo, Dkt. Samia amesema kuwa Wawekezaji waliotelekeza mashamba na viwanda vya zao la chai wilayani Rungwe watanyang’anywa na kuvirejesha kwa wananchi chini ya usimamizi wa Vyama vya Ushirika.
Agizo hilo limetolewa na Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akijibu kilio cha wananchi wa eneo hilo kilichotolewa na wabunge wateule wa Busokelo, Lutengano Mwalwiba na Jimbo la Rungwe Magharibi Anthony Mwantona katika mkutano wa kampeni za CCM kwenye Uwanja wa Tandale Tukuyu Mjini Septemba 5, 2025.
Amesema imeundwa kamati inayoshirikisha viongozi wa serikali na wawekezaji wa kampeni ya Watco na Mohamed Enterprises ili kupata suluhisho la utata huo.
Dkt. Samia amesema kabla ya kuchukua Hatua ya kuwanyang’anya mashamba na viwanda hivyo ameagiza wawekezaji hao kulipa haraka madeni wanayodaiwa na wakulima na wafanyajazi wao.
Aidha, Dkt. Samia ambaye muda wote alikuwa akishangiliwa na Wananchi waliofurika uwanjani hapo, amesema ili walipe haraka madeni hayo umeandaliwa utaratibu nzuri kukopeshwa Fedha na mabenki.
Amesema, Serikali iko mbioni kujenga vituo 50 vyenye mitambo ya ubaridi wa kuhifadhia Matunda ya parachichi kabla ya kusafirisha kuuza Nje ya Nchi. Viwili vinajengwa walayani Rungwe.
Amesema vituo hivyo vitakuwa na uwezo wa kuhifadhia parachichi kwa miezi mitatu kabla ya kusafishwa, lengo likiwa ni kulinda bei ya zao hilo inayobadilika mara kwa mara kutokana na wakati mwingine kuwa mengi katika masoko ya nje.
Aidha, amesema kuwa serikali anayoiongoza imetoa miche milioni moja kwa bei ya ruzuku, lakini vilevile itatoa bure dawa aina ya Coper ya kunyunyizia kwenye miche hiyo ili kuongeza uzalishaji wa zao hilo.
Tanzania ni ya tatu kwa uzalishaji wa zao hilo, ya kwanza ikiwa Afrika Kusini na Kenya.
Amesema endapo Wananchi watamua kumpa ridhaa tena ya kuongoza Nchi kwa miaka mingine mitano kwa kumchagua katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 29, 2025, atahakikisha anakamilisha miradi yote ya Maendeleo iliyomo katika Ilani ya Chama hicho.