DKT. SAMIA AAHIDI MAKUBWA UYUI, IGALULA

ccmkwanza
2 Min Read

MGOMBEA Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameahidi kujenga tanki kubwa la maji lenye ujazo Lita miliini moja ili kutatua tatizo la maji katika Kata nne wilayani Uyui, Tabora.

Ahadi zingine alizozitoa ni ujenzi wa barabara ya Tabora- Isenga na Ndono – Makazi, fedha za ujenzi wa daraja la Loya tayari fedha zimetengwa na kwamba likikamilika anataka wananchi wapite kwa raha hata wakati wa mvua.

Dkt. Samia ametoa ahadi hizo katika mkutano wa Kampeni  uliofanyika Ilolangulu , Uyui, mkoani Tabora Septemba 11, 2025.

.Aidha, Dkt. Samia amewapongeza wakulima wa Tumbaku kwa kuongeza uzalishaji wa Tumbaku kutokana na Serikali kutoa mbolea ya Ruzuku.

Amewaahidi wakulima wanaodai malipo yao kuwa wavute subira Serikali kupitia Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe yupo kwenye mazungumzo na kampuni mbilli zinazodaiwa muda si mrefu watalipwa.

Amesema tatizo hilo la madeni litapungua kutokana na jitihada za Serikali kuongeza kampuni nyingi za kununua Tumbaku.

Aidha, Dkt. Samia amesema akichaguliwa katika Mkutano Mkuu Oktoba 29, 2025 na kupata ridhaa ya kuongoza Nchi atahakikisha anakamilisha miradi mbalimbali ya maendeleo ya miundombinu ya maji, afya, elimu,  nishati na mingineyo.

‎Akiwa katika mikutano hiyo, Dkt. Samia anajinadi kwa kuelezea mafanikio makubwa ya maendeleo yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita katika wilaya hizo, pia kutoa ahadi ya utekelezaji wa miradi mbalimbali.

‎Pamoja na kuelezea kwa undani Ilani ya uchaguzi ya chama hicho, Dkt. Samia ambaye mgombea wake mwenza ni Dkt. Emmauel Nchimbi, ametumia fursa hiyo kuwanadi wagombea ubunge na madiwani wa chama hicho. Jana amefanya kampeni katika Mji wa Manyoni, Ikungi na Singida Mjini.

‎Baada ya uzinduzi wa kampeni kwenye Uwanja wa Tanganyika Packers, Kawe Jijini Dar es Salaam, leo Mgombea huyo ameingia kwa kishindo mkoa wa Nane wa Tabora baada ya kufanikisha kwa kiwango cha hali ya juu  kampeni katika mikoa ya   Morogoro, Dodoma, Songwe, Mbeya, Njombe, Iringa na Singida.

Share This Article
Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *