Sehemu ya wananchi wakiwa katika mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM,Dkt Samia Suluhu Hassan Kigoma Mjini, Septemba 14, 2025.




Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan asubuhi hii anahitimisha kampeni zake katika Mkoa wa Kigoma baada ya jana kufanya Uvinza, Kasulu na Buhigwe.
Kama kawaida katika mkutano mkubwa utakaofanyika Kigoma Mjini ataelezea mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha uongozi wake wa miaka minne na kutoa ahadi za utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani humo.
Kigoma ni kati ya mikoa michache sana ambayo ina miradi mingi sana ya maendeleo. Ndani ya miaka 4 ya Rais Samia mkoa huo umepokea zaidi ya Sh Trilioni 11 kwenye sekta mbalimbali za maendeleo
Baadhi ya miradi mikubwa ya maendeleo inayoendelea na utekelezwaji mkoani Kigoma ni hii ifuatayo,
Ujenzi wa Barabara Kuu za lami zaidi ya km 420 zikiwemo za Kibondo-Mabamba na Kibondo-Marongwe
Ujenzi wa Barabara za mitaa km 10 chini ya Tactic
Ujenzi na Ukarabati wa Bandari ya Lagosa,Kibirizi
Ujenzi wa meli Mpya na Chelezo ya Kuundia meli
Ukarabati wa meli za mv Sangara na Mv Liemba Ziwa Tanganyika
Ujenzi wa Station kuu ya Sgr Kigoma
Ujenzi wa SGR Tabora-Kigoma(Main Camp ni Uvinza-Kigoma)
Ujenzi wa Soko Kuu la Mwanga na soko la Katonga via Tactic
Ujenzi wa Tawi la Chuo Kikuu Cha Muhimbili
Ujenzi wa Tawi la Chuo Cha Uhasibu TIA
Upanuzi wa Chuo Cha Taifa Cha Hali ya hewa na Ufungaji wa radar
Ujenzi wa Hospital ya Rufaa ya Kanda ya Magharibi
Ujenzi,ukarabati na upanuzi wa uwanja wa Ndege wa Kigoma (Gombe-Mahare International Airport)
Ujenzi wa njia kubwa ya kusafirisha Umeme wa Kv 400 Nyakanazi-Kidahwe
Ujenzi wa Tawi la BoT Kanda ya Magharibi (Usanifu unaendelea)
Ujenzi wa Katosha Dry Port
Ujenzi wa meli mpya ya abiria na mizigo
Ujenzi wa meli ya abiria
Ujenzi wa Chuo Cha Umahili wa Tehama Buhigwe
Miradi kedekede ya maji ya zaidi ya Sh. Bilioni 429
Ujenzi wa Malagarasi Hydropower Project
*Ujenzi wa kiwanda kipya cha Saruji Cha Tanzania Cement Company ltd
*Mradi wa ujenzi wa Kiwanda Cha Pamba na Kiwanda Cha Sukari Kasulu.