JITOKEZENI KWA WINGI BILA HOFU SIKU YA KUPIGA KURA OKTOBA 29 – DKT. SAMIA

ccmkwanza
1 Min Read

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Dkt. 𝗦𝗮𝗺𝗶𝗮 𝗦𝘂𝗹𝘂𝗵𝘂 𝗛𝗮𝘀𝘀𝗮𝗻 ametoa wito kwa watanzania kushiriki kampeni za uchaguzi mkuu kupitia chama hicho cha CCM kwa kushiriki kikamilifu kwenye mikutano ya kampeni si tu ya Urais bali kwa wabunge na madiwani.

Dkt. Samia amesema kuwa sambamba na kushiriki mikutano hiyo, amewataka Watanzania wajitokeze kwa wingi kwenda kupiga kura siku ya Oktoba 29 na kuwaomba waendelee kuiamini CCM kwa kumpigia kura yeye kwenye nafasi ya Rais, kuwapigia wabunge na madiwani wanaotokana na chama hicho.

Amewatoa hofu kwamba siku hiyo wasiwe na wasiwasi wowote kwani vyombo vya ulinzi na usalama vimejiandaa, viko imara kinachotakiwa ni kwenda kwa wingi kupiga kura na kurejea salama nyumbani..

Ameyasema hayo leo tarehe 28 Septemba 2025 kwenye mikutano yake ya kampeni hizo za Urais akiwa mkoani Pwani.

Share This Article
Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *