
Na Richard Mwaikenda, Geita
CHAMA cha Wachimba Madini Tanzania (FEMATA) chenye zaidi ya wanachama mil. 6 wameahidi kumpigia kura Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Jamhuri ya Muungano wa Jamhuri wa Tanzania, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa sababu ameiheshimisha sekta ya madini nchini.
Ahadi hiyo imetolewa kwa niaba yao na Mwenyekiti wa chama hicho. John Bina katIka mkutano wa Kampeni za Mgombea huyo kwenye Uwanja wa Bombambili Geita Mjini Oktoba 13, 2025.
“Mimi leo nazungumza kwa niaba ya wachimbaji wote nchini; wachimbaji wa mchanga. Kokoto, mawe, chumvi, kifusi kila aina ya madini yapatayo 250, wameniambia watakuchagua Oktoba 29,”
“Na ni kwanini wameamua kukuchagua, ni kwa sababu umewaheshimisha, umewapa heshima. Sababu gani? hapo zamani familia ziliamini kila anayechimba madini amepotea.” Amesema Bina huku akishangiliwa.
“Lakini sasa nikumbie Mheshimiwa Rais, hivi sasa hata tukipita mjini tunaheshimiwa.”
La pili walilomuamba wachimbaji wamuambie Rais kwamba wako tayari kumlinda kwa wivu sana, sababu Mgombea huyo wa CCM amewafanyia vitu kwa wivu sana.
Jambo lingine kubwa alilowanyia ni kuwapatia wachimbaji leseni zisizo na mipaka pamoja na kupunguza kwa kissi mikubwa kodi na ushuru.