TUMIENI MVUA ZA MASIKA KUPANDA MITI-SINENE

ccmkwanza
1 Min Read

Balozi wa Mazingira,Ahidi Sinene ametoa wito kwa wananchi kuzitumia mvua za masika zinazoendeleo kupanda miti kwa ajili ya kuhifadhi mazingira na kwani jambo hilo ni ibada kama ibada zingine na kwamba kutotunza mazingira ni dhambi kama zilivyo dhambi zingine.

Ameyasema hayo aliposhiriki pamoja na wanafunzi na walimu kupanda miti zaidi ya 100 aliyoitoa katika Shule ya Sekondari Umonga jijini Dodoma Machi 16, 2026.Kila anapokwenda kupanda miti amekuwa Sinene akihamasisha kila mwananchi kuwajibika kupanda angalau kwa uchache miti mitano katika eneo lake kuifanya Dodoma kuwa ya Kijani.

Balozi huyo wa Mazingira ambaye pia ni Mjumbe mstaafu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dodpoma, amekuwa na tabia kupanda miti katika maeneo mbalimbali mkoani humo ambapo Januari 16, 2021, Sinene alikwenda kushiriki kupanda miti katika Shule ya Sekondari Bihawana, Kata ya Mbabana nje kidogo ya Jiji la Dodoma ambapo walipanda miti 230 ikiwemo ya matunda.

Balozi wa Mazingira,Ahidi Sinene akipanda mti.

Wanafunzi wa shule hiyo wakishiriki kupanda miti.

https://www.youtube.com/embed/FQbxzwNOAHMIMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA -0754264203

Share This Article
Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *