Mbunge wa Mbeya Mjini, Patrick Mwalunenge amewatetea na kuwapambania bungeni waendesha bodaboda 120 ambao pikipiki zao zimekamatwa na Askari wa Wakala wa Usimamizi wa Misitu Tanzania (TFS) kwa tuhuma za kusafirisha mkaa jijini Mbeya.
Ameishauri Wizara ya Maliasili na Utalii badala ya TFS kuwakamata iwawezeshe kuwapa mitaji ya kufuga nyuki kwa ajili ya asali katika msitu wa Kawetele ili waache kusafirisha mkaa bali wawe wanafuga nyuki na vilevile kusaidia kuutunza msitu huo. Zaidi ya vija 300 wako tayari.
Pamoja na mambo mengine,Mwalunenge ameyasema hayo alipokuwa akichangia mjadala wa makadirio ya Bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha wa 2026/2027 bungeni Dodoma Mei 19, 2026.