Katibu wa Bunge, Baraka Leonard ametangaza majina ya matatu ya watanzania walioteuliwa kugombea ujumbe wa Bunge la Afrika Mashariki katika uchaguzi utaofanyika Jumatatu Mei 4, 2026 bungeni Dodoma.
Majina hayo yametangazwa mbele ya vyombo vya habari jijijini Dodoma Aprili 30, 2026 baada ya kuchujwa katika kikao cha wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Pius Msekwa.
Wagombea hao ni; (a) Ndg. Fatuma Abdallah Kange (b) Ndg. Cosato David Chumi (c) Ndg. Kambarage Masato Wasira