MAANDALIZI YA MKUTANO MKUU MAALUMU WA CCM YAPAMBA MOTO DODOMA

ccmkwanza
2 Min Read

CHAMA Cha Mapinduzi  (CCM) kinaanza kujenga  la kisasa la Makao Makuu jijini Dodoma linalojengwa karibu na Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete.

Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuweka Jiwe la Msingi la Jengo la Makao Makuu ya CCM Mei 28 mwaka huu.

Hayo yameelezwa na Katibu  wa Itikadi,Uenezi na Mafunzo CCM, CPA Amos Makalla, alipokuwa akuzungumza na vyombo vya habari jiji Dodoma Mei 24, 2025, kuhusu maandalizi ya Mkutano  Mkuu maalumu  wa chama hicho  unaotarajiwa kufanyika Mei 29-30 katika ukumbi wa Jakaya Kikwete. 

CPA Makalla amesema kuwa Jengo hilo litakuwa la kisasa ambalo litakuwa na huduma zote muhimu na litaendana na hadhi ya CCM ambayo kwa sasa inawanachama zaidi ya milioni 11.

“Tunajenga jengo la Makao Makuu karibu na  Jengo hili ( Jakaya  Kikwete) ambalo litakuwa na facilities zote CCM ni Chama kikubwa Tanzania pamoja na Afrika,tumeona umefika wakati wa kuwa na jengo lenye facilities zote kumbi za mkutano, parking kwa sababu  Chama hichi ni kimbilio la  wananchi,”amesema  Makalla.

Aidha, amesema kuwa maandalizi kwa ajili ya Mkutano Mkuu maalumu  wa Chama cha Mapinduzi (CCM) yamekamilika na  unatarajiwa kufanyika Mei 29-30 katika ukumbi wa Jakaya Kikwete na utahudhuriwa na wajumbe 2000 wa mkutano Mkuu kutoka mikoa yote nchini..

Katibu  wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM Taifa, CPA Amos Makalla,akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano huo.


Makalla akikagua maandalizi katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete.

Share This Article
Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *