Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge na watu wenye ulemavu), pRofesa Paramagamba Kabudi amesema kuwa kwa mujibu wa sheria za nchi kisheria hairuhusiwi matumizi ya aina yoyote ya bangi kama vile dawa, chakula. Ameyasema hayo alipokuwa akijibu maswali ya wanahabari katika mkutano alipokuwa akitoa taarifa ya Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya kuhusu hali ya dawa za kulevya nchini ya mwaka 2025 iliyowasilishwa bungeni leo Mei 29, 2026.


