LETENI HARAKA FEDHA ZA KUKAMILISHA UJENZI WA VITUO VYA AFYA KILINDI – MHANDO

ccmkwanza
2 Min Read

Mbunge wa Jimbo la Kilindi, Saleh Mhando bungeni Dodoma Juni 4, 2026, kwamba lini Serikali itapeleka fedha za Awamu ya Pili kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa Vituo vya Afya vya Vuyu, Mswaki na Negero katika Jimbo la Kilindi?

Majibu yamejibiwa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Rajabu Seif kama ifuatavyo;

Serikali imeendelea kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya vya katika Kata za kimkakati kote nchini. Katika kipindi cha miaka 5 Serikali imejenga jumla ya vituo vya afya 487 vikiwemo vituo vya afya vya Vuju na Mswaki na Negero katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi.

, Serikali imefanya tathmin na kuainisha jumla ya vituo vya afya 364 vyenye upungufu wa miundombinu muhimu. Aidha, vituo 111 vimetengewa bajeti ya shilingi bilioni 23.37 mwaka 2026/27 kwa ajili ya ukamilishaji ikiwemo halmashauri ya Wilaya ya Kilindi ambayo imetengewa shilingi milioni 200 kukamilisha vituo vya afya Vuju na Mswaki.

Aidha, kituo cha Afya Negero ni kati ya Vituo vya Afya 120 vya kimkakati vilivyopokea shilingi milioni 250 kupitia bejeti ya nyongeza ya mwaka wa fedha 2024/25. Ujenzi umehusisha jengo la Kuhudumia wagonjwa wa nje (OPD), choo cha nje na kichomea taka ujenzi upo hatua ya ukamilishaji.

Serikali itaendelea kutenga fedha kwa awamu na kukamilisha ujenzi wa miundombinu ya vituo vya afya ili viweze kutoa huduma muhimu ikiwemo huduma za upasuaji wa dharura kwa akinamama wajawazito.

Share This Article