RAIS SAMIA ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI MSIBA WA MKURUGENZI MTENDAJI WA TANESCO

ccmkwanza
1 Min Read

 SALAMU ZA RAMBIRAMBI 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan  amemtumia salamu za rambirambi Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe.  Dkt. Doto Biteko kufuatia kifo cha aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika La  Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Gassima Nyamo-Hanga pamoja na dereva  wake Muhajir Mohamed Haule.  

Marehemu Nyamo-Hanga na dereva wake wamefariki usiku wa kuamkia leo tarehe  13 Aprili, 2025 katika ajali ya gari iliyotokea katika Wilaya ya Bunda, Mkoani Mara.  

Rais Dkt. Samia anawapa pole Wizara ya Nishati, TANESCO, familia, ndugu, jamaa  na marafiki wa marehemu Nyamo-Hanga na Haule. 

Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu Nyamo-Hanga na Haule mahala pema  peponi, Amina. 

Sharifa B. Nyanga 

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu

Share This Article
Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *