BARABARA HIZI NJOMBE NI MUHIMU KIUCHUMI, ZIJENGWE – MWANYIKA

ccmkwanza
1 Min Read

Mbunge wa Njombe Mjini, Deodatus Mwanyika ameitaka Serikali kukamilisha haraka ujenzi wa barabara ya mkakati ya Itoni- Lusitu pamoja na barabara ya Makambako, Njombe hadi Songea kwani zote zina umuhimu mkubwa kiuchumi.

Aidha, ameitaka serikali kuheshimu sheria iliyotungwa na Bunge ya kuanzisha Mfuko wa Barabara na kusisitiza kwamba fedha za mfuko huo zitumike mahsusi kwa ujenzi wa barabara nchini na si vinginevyo.

Ameyasema hayo alipokuwa akichangia mjadala wa makadirio ya Bajeti ya Wizara ya Ujenzi kwa mwaka wa fedha wa 2026/2027 bungeni Dodoma Mei 20, 2026.

Share This Article